Uzinduzi wa promosheni yaTECNO Vimba Season umefanyika rasmi tarehe 4/8/2020 huku hafla hiyo ikihudhuriwa nawasanii maarufu wa tamthiliya ya HUBA ambayo huoneshwa na king’amuzi cha Dstv.
Promosheni hiyo ya ‘VimbaSeason’ inalenga kuwapatia wateja wa TECNO CAMON15 na Spark5 zawadi mbalimbaliikiwemo seti ya king’amuzi cha Dstv kilicholipiwa chaneli za kifurushi chafamilia kwa mwezi mzima, pia wateja wa simu hizi watapata nafasi ya kuingia mojakwa moja kwenye droo ya shindano lazawadi kubwa ya gari.
Akizungumza wakatiwa hafla ya uzinduzi huo, meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed alisemapromosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Vimba Season ambayo hufanyikamara moja kila mwaka.
“Leo kwa mara nyinginetena tumewaletea msimu wa promosheni ya Vimba Season na kwa mwaka huu simuambazo zitaambatana na zawadi ni TECNO CAMON 15 na Spark5. Kwahiyo Mteja yeyoteatakayenunua CAMON15 au Spark 5 ana uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye drooyetu kubwa ya kushinda gari” alisema Bi. Mariam.
Bi Mariam aliongeza kuwa,“Pia tuna Dstv kwa mara nyingine tena, ukinunua simu hizi CAMON15 au Spark5unapata Dstv na promosheni yetu inaanza rasmi leo nchi nzima.”
Kwa upande wake menejamasoko wa TECNO Bw. William Motta alisema kuwa promosheni hiyo itafanyika kwamuda wa mwezi mzima nchini kote katika maduka ya TECNO na kuwaomba wateja wotewa TECNO na watanzania kwa ujumla kutoikosa kwani ni fursa kwa kila mmoja.
|
30267393 19 #
MBN sms tunazotuma zinachelewa kuwafikia?