Kampuni ya simu TECNO yazindua rasmi TECNO Spark 5 pro. Uzinduzi wa simu hiyo umefanyika Kidimbwi Beach tarehe 18/10/2020 na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo komediani maarufu Jaymond na wadau wa simu za TECNO.
Uzinduzi wa Spark 5 pro ulifanyika katika mfumo wa party ambapo DJ Maphorissa kutoka South Africa alitoa burudani yakutosha na kuufanya uzinduzi wa Spark 5pro kuwa wa aina yake.
“Spark 5 pro sio simu ya kwanza kwa kampuni ya TECNO kuzinduliwa kwa mfumo wa party na hii imejirudia kwasababu Spark 5 pro ni simu yenye kutulenga vijana wa kileo na ili kuweza kutufikia kwauharaka zaidi basi ni lazima kutumia njia zetu kama hivi
Baadhi ya sifa zinazopatikana katika simu hii ya TECNO spark 5pro ni uwezo wa simu hii kuwa na ukubwa wa memory ya GB 64ROM + GB 3RAM, selfie ya megapixel 8 na kamera ya nyuma ni megapixel 16M+2M+2M+AI Lens, battery ya ujazo wa mAh 5000, alisema msanii maarufu wa comedy Jaymond ambaye ndio mgeni mualikwa katika uzinduzi huo”.
“Uzinduzi wa Spark 5 pro ni waaina yake sisi kama wateja wa simu za TECNO tumefurahi kuona namna TECNO inavyotujali na kututhamini, tumekula tumekunywa lakini pia tumepata nafasi ya kupiga picha na mgeni mualikwa alisema Bwana Haji Omary”.
TECNO Spark 5pro sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.
|
30842580 15 #