Ukurasa wa mwanzo > kifungu > Management > General > TECNO CAMON 16s YAZINDULIWA RASMI

TECNO CAMON 16s YAZINDULIWA RASMI

General  |  2020-11-18 10:14 243304

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua rasmi  simu yake mpya toleo la CAMON 16s leo jijiini Dar es Salaam pamoja na kuwatambulisha mabalozi wa simu hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, meneja mahusianowa kampuni hiyo bwana Eric Mkomoya amesema simu hiyo sio tu imelenga kurahisisha mawasiliano bali kuleta mapinduzi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazotegemea zaidi  teknolojia hasa upande wa kamera.

“Pamoja na kwamba simu ni kifaa cha mawasiliano lakini kutokana na sifa za TECNO CAMON 16s mtumiaji akiitumia kwa ufanisi itampa maslahi makubwa kuanzia wafanyabiashara, wajasiriamali ,wasanii,  wafanyakazi maofisini na hata wanafunzi wa vyuo vikuu” Amesema Mkomoye.

Image 1.jpg
Msanii wa bongo Muvi ElizabethMichael (LULU) akipiga selfie kwa TECNO CAMON 16s
Akibainisha baadhi ya sifa za simu hiyo Mkomoye amesema TECNO CAMON 16s ina kioo kikubwa chenye inchi 6.6, kamera nne nyuma na huku kamera kuu ikiwa na 48MP, amesema ukubwa wa kamera hiyo unaiwezesha Camon 16s kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu ikiwezeshwa na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI.

Image 2.jpg
Mwonekano wa mbele nanyuma wa TECNO CAMON 16s   

“Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu ya TECNO CAMON 16s ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwamakwama” Aliongeza Mkomoye.

Image 3.jpg
Mtangazaji Omary Tambwe katikapozi akipiga selfie kwa kutumia TECNO CAMON 16s
Image 4.jpg
Mlimbwende Jihan Dimack na MuigizajiLulu wakitazama selfie zilizopigwa na TECNO CAMON 16s.
Akiwatambulisha mabalozi wa TECNO CAMON 16s, Mkomoye alisema  mabalozi hao watashirikiana na kampuni hiyo ili kurahisisha kufikisha ujumbe kwa  wateja na watu wote wanaopenda kutumia simu zenye teknolojia ya kisasa. Mabalozi hao ni pamoja na  Omary Tambwe,  Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye ni msanii wa bongo muvi pamoja na Miss University Bi. Jihan Dimack.

Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram;  

  • Penda(10)
  • Shiriki
Itabidi uingie kabla ya kujibu Ingia | Jisajili

polla 21 #

bei ya cammon primer nish ngapi
2021-2-18 11:19 Penda(0)

30620991 20 #

hi guys, i am new to this group, hopefully I will learn a lot from you.
2021-1-29 08:50 Penda(0)

30571583 19 #

shingapi
2021-1-21 20:17 Penda(0)

257009152234 18 #

nikiitaji nitapata wp
2021-1-18 16:28 Penda(0)

30533597 17 #

Ustedes Dos Si Que Estan Muy,Pero Muy Lindas Preciosas Bellesas Hermosas de la VIDA
2021-1-11 20:32 Penda(0)

30533597 16 #

Tu Si Que Eres una Preciosura Hermosa De La Vida De Cualquiera Que Este A Tu Lado
2021-1-11 20:29 Penda(1)

ushiyegos 15 #

hizo siyo camon 16s
2021-1-7 00:45 Penda(1)

ushiyegos 14 #

haina standard lounch.. sijui naipataje..
2021-1-3 15:15 Penda(1)

ushiyegos 13 #

iko viziur mno
2020-12-26 15:08 Penda(2)

waku7bisha

Msimamizi

Fuata Ongea

© 2021 TECNO Mobile