Chapisho hili lilihaririwa kwa mara ya mwisho na TECNO SPOT TZ mnamo 2020-11-21 11:52
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imetangaza kuanza rasmi promosheni ya Camon16Billboard Star ambayo itawawezesha wafuasi wake wa kurasa za mtandaoni pamoja na wateja kwa ujumla kujinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi milioni moja, kupata nafasi ya kuwekwa kwenye bango kwa muda wa wiki kadhaa pamoja na kupata nafasiya kwenda ziara ya Camon 16.
Picha ya msanii LULU ikionesha namnamwonekano wa picha ya mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaa kwenyebango
Akizungumza wakati wa kuitambulisha kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, meneja masoko mtandaoni Bi.Salma Shafi amesema wameandaa kampeni hiyo maalum kwa ajili ya wateja na wafuasi wao wa kwenye kurasa zao mtandaoni.
“Hii ni kampeni ambayo inamtaka mshiriki kupiga picha yoyote kwa ubunifu yaani ‘creative photo’ . picha inaweza kuwa ya mtu au kitu yenye ubunifu kwa kutumia TECNO CAMON 16 au simu yoyote ya toleo la TECNO CAMON na ahakikishe ameweka watermark ili kutambulisha picha imepigwa kwa simu ya toleo la TECNO CAMON. Akishapiga picha anatakiwa aposti kwenye akaunti yake ya Instagram kwa hashtag #Camon16BillboardStar” amesema Bi. Salma
Picha ya mtangazaji Omary Tambweikionesha namna mwonekano wa picha ya mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaakwenye bango Bi. Salma ameongeza kuwa Kupitia kampeni hiyo ya ‘Camon 16 billboard star’ ambayo itadumu kwa muda wa wiki moja na mwishowe watachaguliwa washindi watano na kuwa reposted kwenye ukurasa wa Instagram ‘tecnomobiletanzania’ kisha kufanyiwa mchujo kwaajili ya kupata mshindi mmoja.
Picha ya miss University JihanDimack Ikionesha namna picha ya mshindi wa itakavyokaa kwenye bango Kampeni hiyo ya Camon16 BillboardStar, itafuatana na ziara ya Camon16 ambapo washindi watapata nafasi yakutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi za Taifa ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro.
|
ts30197291 2 #