Machapisho yanayopendekezwa

TECNO CAMON 16s YAZINDULIWA RASMI

General

waku7bisha | 2020-11-18325234

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua rasmisimu yake mpya toleo la CAMON 16s leo jijiini Dar es Salaam pamoja na kuwatambulisha mabalozi wa simu hiyo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, meneja mahusianowa kampuni hiyo bwana Eric Mkomoya amesema simu hiyo sio tu imelenga kurahisisha mawasiliano bali kuleta mapinduzi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazotegemea zaiditeknolojia hasa upande wa kamera. “Pamoja na kwamba simu ni kifaa cha mawasiliano lakini kutokana na sifa za TECNO CAMON 16s mtumiaji akiitumia kwa ufanisi itampa maslahi makubwa kuanzia wafanyabiashara, wajasiriamali ,wasanii,wafanyakazi maofisini na hata wanafunzi wa vyuo vikuu” Amesema Mkomoye. Msanii wa bongo Muvi ElizabethMichael (LULU) akipiga selfie kwa TECNO CAMON 16sAkibainisha baadhi ya sifa za simu hiyo Mkomoye amesema TECNO CAMON 16s ina kioo kikubwa chenye inchi 6.6, kamera nne nyuma na huku kamera kuu ikiwa na 48MP, amesema ukubwa wa kamera hiyo unaiwezesha Camon 16s kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu ikiwezeshwa na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI. Mwonekano wa mbele nanyuma wa TECNO CAMON 16s “Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu ya TECNO CAMON 16s ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwamakwama” Aliongeza Mkomoye. Mtangazaji Omary Tambwe katikapozi akipiga selfie kwa kutumia TECNO CAMON 16sMlimbwende Jihan Dimack na MuigizajiLulu wakitazama selfie zilizopigwa na TECNO CAMON 16s.Akiwatambulisha mabalozi wa TECNO CAMON 16s, Mkomoye alisemamabalozi hao watashirikiana na kampuni hiyo ili kurahisisha kufikisha ujumbe kwawateja na watu wote wanaopenda kutumia simu zenye teknolojia ya kisasa. Mabalozi hao ni pamoja naOmary Tambwe,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye ni msanii wa bongo muvi pamoja na Miss University Bi. Jihan Dimack. Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram; https://cutt.ly/VgDoVDQ
Soma zote >>

Umeona wapi au kusikia taarifa kuhusiana na Camon 15?

waku7bisha | 2020-07-021155323

CAMON 15 Series
Habari ndugu wadau wa TECNO Spot. Tunahitaji kusikia maoni yako kua ni wapi umesikia au kuona taarifa kuhusiana na Camon 15. Gusa hii link hapa chini kuweka jibu lako https://forms.gle/HxBzu5ndmbmZKTaa7 Asante. Soma zote >>

HiOS CREATIVE PHOTOGRAPHY CONTEST

HiOS Official Account | 2020-06-06511896

HiOS
Habari T-Mashabiki, Mtu mwenye busara wakati mmoja alisema, "Picha imedhamiriwa na mpiga picha, sio kamera." Na alikuwa sahihi. Sasa ni wakati wa tena kurudisha akili za ubunifu! Tunayo kazi rahisi kwako. Rahisi sana. Unayohitaji kufanya ni kuchukua picha ya ubunifu ya kifaa chako cha Tecno! Ni rahisi! Sio haraka sana! Tunahitaji pia uichukue kwa ubunifu. Kwa hivyo, kabla ya kubonyeza kitufe cha kufunga, fikiria njia ya ubunifu ya kuchukua picha ya simu… Wacha mchezo uanze! Miongozo ya shughuli: Mzunguko wa kwanza wa shughuli ungechaguliwa kulingana na ubunifu. Majaji wangechagua picha 18 za ubunifu kutoka kwa nchi zote 11 zilizowakilishwa kwenye T-Spot (Nigeria, Kenya, Pakistan, Ghana, Mali, India, Senegal, Guinea, Tanzania, Bangladesh) na kuziweka ili wapigie kura. Kura ya Juu 5 iliyo na kura ya juu kabisa ni mshindi! Uwasilishaji wa viingilio ni kuanzia tarehe 5 Juni hadi tarehe 14 Juni, 2020. Upigaji kura kwa ya juu 5 huanza tarehe 15 Juni na kumalizika Juni 16, 2020 Tangazo la washindi mnamo Juni 17, 2020 Thawabu ya washindi mnamo Juni 20, 2020 Kanuni: Sheria na Masharti: • Kuingia kwako lazima iwe chini ya uzi huu • Kifaa lazima kiwe kifaa cha Tecno. • Picha lazima iwe ya kipekee kwako. Picha za mtandao zitastahiki • Lazima uwe unafuata HiOS kwenye Jukwaa zote za Media Jamii na pia kwenye Tecno Spot. (@HiOSGlobal kwenye media zote za kijamii isipokuwa Instagram, @HiOS_Global). Tungeuliza kwa dhibitisho kabla washindi hawajalipwa • Pata marafiki wako kupenda chapisho lako. Vipendwa vya juu zaidi havilingani kushinda. Zero zinapenda haziwezi kuhitimu • HiOS ina haki ya kukatisha kiingilio chochote ambacho hakifuata sheria • HiOS ina haki ya kubadilisha sheria wakati wowote wakati wa mashindano Hakikisha unafuata rasmi ya HiOS kwa habari za hivi karibuni na mashindano Soma zote >>

SIMU YENYE KAMERA TANO (TECNO SPARK 5) YAACHIWA RASMI

waku7bisha | 2020-06-02373139

General
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezinduasimu yake mpya TECNO SPARK 5 yenye kamera tano ambapo uzinduzi huo ulifanyika Jijini Dar es Salaam moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii zikiwemo kurasa za mitandao ya kijamii za TECNO. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed alisema uzinduzi wa simu hiyo umekuja ukiwa umeambatana na kifurushi cha zawadi kwa wateja yaani (Gift Box) ambayo ni maalum kwaajili ya mteja yeyote anayenunua TECNO SPARK 5.“Tumekuja na vitu spesho sana kwaajili ya wateja wetu tuna zawadi nyingi sana tofauti tofauti ambazo mteja wetu yeyotewa TECNO SPARK 5 atakutana nazo na hapa kuna Gift Box na ndani yake kuna vitu tofauti tofauti zikiwemo kibeba funguo(Key holder), selfie stick,chupa, headphonepamoja na kifuko maalum cha kuhifadhia simu unapokuwa mazoezini” Alisema Bi. Mariam Bi. Mariam aliongeza kuwa zawadi hizo zitatolewa kwa mteja yeyote atakayenunua TECNO SPARK 5 na kwamba tayari promosheni hiyo imeanza rasmi nchi nzima katika maduka yote ya TECNO. Wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya TECNO SPARK 5 inayosifika kwa kamera5 zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha mahali popote hata gizani, TECNO pia ilimtambulisha rasmi Bw. Jonijo ambaye ni mtangazaji maarufu wa radio, kuwa balozi wa TECNO SPARK 5. Kwa upande wake balozi huyo wa TECNO SPARK 5 alisema amekuwa mfuatiliaji mzuri wa matoleo ya TECNO SPARK, kuanzia SPARK 3, SPARK 4 mpaka sasa SPARK 5.“Mchongo wa TECNO SPARK 5 umekaa poa sana, unajua TECNO sasa hivi wamerahisisha maisha kwasababuSPARK 5 kuna kioo nimekutana nacho kina maajabu yaani ni inchi 6.6”, SPARK 5 pia ina kamera 5 kwaajili ya picha na video kali wakati wowote” Alisema Jonijo.“Unajua kamera hizi zinavyofanya kazi hata lile tone la maji unaweza kulinasa kwa kamera ya TECNO SPARK 5, na kitu kizuri zaidi betri yake ni 5000mAh hiki kitu ni balaa habari ya kuchaji simu kila siku sahau, hii ukichaji mara moja unakwenda nayo siku 3” Aliongeza Jonijo.Tayari TECNO SPARK 5 ipo kwenye maduka ya simu mikoa yote Tanzania bara na visiwani huku bei yake ikiwa ni rafiki katika kipindi hiki. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania. Soma zote >>

Eid Mubarak

waku7bisha | 2020-05-246722

General
Tunawatakia Eid njema yenye amani na furaha. Eid Mubarak. Soma zote >>

TECNO Yaja Kivingine, Sasa Kuzindua Simu Mpya Yenye Kamera 5

waku7bisha | 2020-05-22232586

Others
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua simu yakempya aina ya TECNO SPARK 5 yenye kamera 5 Ijumaa ya tarehe 22/05/2020 kwa njia ya mtandao, ikiwa ni mara ya pili kuzindua kwa njia hiyo ya mtandao ambayo kwa mara ya kwanzailitanguliwa na TECNO CAMON 15. Akizungumza kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam, afisa masoko wa TECNO mtandaoni Bi. Salma Shafii amethibitisha kuwa ni kweli simu hiyo imezinduliwa kwa njia ya mtandao. “TECNO SPARK 5 ni simu ambayo ina kamera 5 na tumeizindua tayari. Hii imekuja katika wakati muafaka kutokana na kwamba imezingatia ubora, pili imezingatia uchumi wa sasa kwa maana ya bei yake kuwa nafuu sana” Alisema Bi. Salma Simu hiyo mpya ya TECNO SPARK 5 imekuja na kamera nne nyuma na mbele ni moja ambapo kamera yake kuu ya nyuma ina MP13 hukukamera zingine 3 zikiwa namfumo wa AI ambao husaidia kutengeneza mazingira ya upigaji picha vizuri mahali popote, iwe mchana au usiku na mahali pengine popote na hata kwenye mwanga hafifu simu hii hutoa picha nadhifu na inayong’ara katika mwonekano mzuri. “Kwa upande mwingine TECNO SPARK 5 imekuja ikiwa na betri kubwa yenye kutunza chaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kuwa na 5000mAh. Ni simu isiyohitaji kutembea na power bank” Alisema Bi. Salma. Hata hivyo TECNO SPARK 5 imethibitishwa kuwa ni simu ambayo ina skrini kubwa yenye inchi 7 na inamwezesha mtumiaji kutazama video au kucheza gemu bila kutatizika na kwa muda mrefu kadiri anavyotaka. Simu hiyo yenye teknolojia ya kisasa kabisa imekuja ikiwana rangi nne kuu; Ice Jadeite, Spark Orange, Vacation Blue na Misty Grey. TECNO SPARK 5 imekuja ikiwakatika aina tatu;SPARK 5 Pro, SPARK 5 na SPARK 5 Air. Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa simu hiyo ya SPARK 5 ulifanyika katika kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania Soma zote >>

TECNO CAMON 15 YATISHA KIMAUZO

waku7bisha | 2020-05-18322642

CAMON 15 Series
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imebainishwa kuwa ndio kinara kwa Tanzania katika mauzo ya simu yake mpya ya TECNO CAMON 15 huku ikiwa na muda wa mwezi mmoja tu tangu izinduliwe na kuingizwa sokoni rasmi. Meneja mauzo wa kampuni ya simu ya TECNO Bi. Mariam Mohamed ameeleza kuwa ubora wa TECNO CAMON 15 na uzingatiaji wa mahitaji ya wateja wao ndivyo vitu vilivyofanya simu hiyo kuuzwa sana ndani ya mwezi mmoja. "Tumezindua CAMON 15 katikati ya mwezi Aprili mwaka huu lakini mpaka sasa tumeweza kuuza CAMON 15 pisi zaidi ya 2500 huku kukiwa bado kuna hitaji kubwa la wateja” Alisema Bi. Mariam. Bi. Mariam aliongeza kuwa, “TECNO tumeaminiwa sana na wateja na sababu kubwa ya kuongoza kimauzo ndani ya mwezi mmoja ni kutokana na ubora wa CAMON 15 ambayo ni simu iliyozingatia soko la sasa na mahitaji ya teknolojia ya kisasa kwa wateja wetu." Meneja Mauzo wa kampuni ya TECNO Bi. Mariam Mohamed akiwa katika moja ya duka kubwa la TECNO jijini Dar es Salaam. TECNO CAMON 15 inayosifika kwa kamera yake,betri, mwonekano na skrini yake. Simu hiyo ina kamera tatu nyuma lensi na flash ambapo kamera kuu ina MP64 huku kamera ya mbele ikiwa na MP32. Ikumbukwe kuwa TECNO CAMON 15 ilizinduliwa katikati ya mwezi Aprili kwa njia ya mtandao huku msanii maarufu wa bongo muvi Elizabeth Michael (LULU) akitambulishwa kama balozi wake. Balozi wa TECNO CAMON 15 Bi. Elizabeth Michael (LULU) akiwa na mchekeshaji maarufu Jaymond katikati ya mwezi Aprili mara baada ya kuzindua CAMON 15 Soma zote >>

TECNO YAACHIA RASMI CAMON 15 SMARTPHONE MPYA

waku7bisha | 2020-04-19594016

CAMON 15 Series
Kampuni ya simu za mkononiya TECNO, imezinduarasmi simu yake mpya CAMON 15 ambayo imesheheni sifa mbalimbali ikiwemokamera ya nyuma yenye MP64 na mbele MP32 ambayo imewekewateknolojiakubwa yenye uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo wiki hii jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii meneja uhusiano wa kampuni hiyo Bwana Eric Mkomoya, alisemasimu hiyo itawasaidia sana watu wanaopendakutumia kamera katika nyanja mbalimbali za maisha wakiwemo wafanyabiashara, wanamitindo, wanaopenda utalii wa kusafiri, wafanyabiashara za mitandaoni, waandishi wa habari pamoja na makundi mengine ya kijamii.“Simu hii TECNO CAMON 15 ina sifa nyingi sana kubwa na zinazoweza kumridhisha mtumiaji, kamera yake ya nyuma ina MP64 na mbele ni MP32 lakini inatunza sana chaji. Kamera ya simu hii ina uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote hata usiku” Alisema Mkomoya. Meneja uhusiano wa kampuni ya TECNO Bwana Eric Mkomoya Aliongeza kuwa TECNO CAMON 15 ni tofauti na simu nyingine kwani hii inapiga picha kwa kuchukua eneo pana zaidi kutokana na kioo chake kikubwa hivyo hata kama mtu anapiga selfie ya zaidi ya mtu mmoja hahitaji kusogeleana kwa karibu hasa kipindi hiki cha janga la maambukizi ya virusi vya corona. Wakati huohuo kampuni ya TECNO ilimtambulisha msanii wa Bongo muvi Bi. Elizabeth Michael maarufu LULU kuwa balozi wa CAMON 15. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Lulu alisema TECNO imefanya kazi nzuri na kwa wakati sahihi kuingiza CAMON 15 sokoni kwani simu hiyo ina uwezo mkubwa sana na anaamini itakata kiu ya watu wanaopenda kutumia kamera kama watu wa tasnia yake akiwemo yeye.“Unajua maisha yetu kwa kiasi kikubwayanategemea picha, wakati wowote na popote tunapokuwa tunafanya kazi zetu, tunategemea picha kupromoti kazizetu , kwahiyo unakuta tunategemea kamera nzuri na yenye uwezo mkubwa, na kamera ya CAMON 15 binafsi nimeipenda sana” Alisema Lulu.Pia Lulu alisema amevutiwa na muudo mzuri wa simu hiyo kutokana na umbo lake kuwa zuri na hivyo yuko tayari kujivunia popote atakapokuwa. Wakatihuohuomeneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamedalizindua promosheni ya TECNO CAMON 15 nchi nzima ambapo kila mtejaatakayenunuaCAMON 15atazawadiwa begi la TECNO au chombo cha kutunziachakula maarufu ‘Lunch box’ ama kupewa vyote kwa pamoja. “Ofa hii ipo mikoa yote kwenye maduka ya TECNO, kwahiyotunawakaribisha sana wateja wote kwenye maduka yetu” Alisema Bi. Mariam. TECNO imefanya uzinduzi wa simu yake kwa njia ya mtandao katikatiya juma ikiwa ni hatua muhimu ya kuepusha mikusanyiko katika kipindi hiki chajanga la Corona. Tayari TECNO CAMON 15 ipo kwenye maduka yote ya simu nchinzima. Soma zote >>

TECNO kuzindua simu mpya CAMON 15 kwa njia ya mtandao

waku7bisha | 2020-04-15171634

CAMON 15 Series
Katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, Kampuni ya Simu za Mkononi TECNO imeandika historia Tanzania kwa kufanya uzinduzi wa simu yake mpya aina ya CAMON15 siku ya Aprili 15,2020 kwa njia ya mtandao ‘Online Launch’ na kuruka moja kwa moja katika mitandao ya kijamii. Akizungumzia kuhusu uzinduzi huo katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo jiijini Dar es Salaam, Afisa Masoko wa TECNO Mtandaoni, Salma Shafi, amesema hiyo itakuwa fursa kwa kampuni hiyo kuwasiliana moja kwa moja na wateja wake na Watanzania kupitia teknolojia ya Intanteti. “Hii sio tu nafasi nzuri kwa TECNO kuwasiliana na wateja wetu na Watanzania moja kwa moja, lakini pia inamaanisha kuwa matumizi ya vifaa vya kielektroniki na teknolojia Tanzania yanakuja katika hatua mpya sawa na simu tutakayoizindua ya CAMON15 ambayo ina teknolojia mpya ya kisasa kabisa ambapo wateja wetu wataweza kushuhudia uzuri wake.,” amesema Shafi. Amesema kuwa wakati wa uzinduzi huo TECNO itatambulisha rasmi toleo la simu yake mpya ya CAMON15 pamoja na teknolojia yake ya kisasa iliyotumika kutengeneza kamera katika simu hiyo pamoja na sifa nyingineAmeongeza kuwa TECNO ambayo ni kampuni kinara yenye teknolojia ya juu katika simu janja “Smartphone” na imekuwa ikiwapandisha kiwango wateja wake kwa kutoa matoleo mbalimbali ya simu kulingana na mahitaji. “Kwa kudhihilisha hilo toleo hili jipya la simu ya CAMON15 imekuja na kamera yenye MP64 nyuma huku ikisaidiwa na kamera nyingine ndogo mbili ili kuongeza ufanisi zaidi katika suala la picha.,” amesema Shafi na kuongeza kuwa;“Kamera ya TECNO CAMON15 ina teknolojia iliyojikita katika kutatua changamoto za kupiga picha kwenye maeneo yenye mwanga hafifu au usiku.Kamera hii imejengewa uwezo wa kuvikabili vizuizi vyote ambavyo hufifisha picha, kutokana na teknolojia hii, picha iliyopigwa na CAMON15 inabaki kuwa bora hata ikikuzwa (zoomed) mara nane..” amesema Soma zote >>

TECNO yathibitisha kuachia CAMON 15 simu yenye kamera ya karne!

waku7bisha | 2020-04-14131463

CAMON 15 Series
Baada ya uvumi wa siku kadhaa kuhusu kampuni ya simu itakayoleta teknolojia kali ya kamera ya simuinayotarajiwa na wajuzi wa kutumia simu janja mwaka huu 2020, kampuni ya simu za mkononi ya TECNO tayari imethibitisha kuwa itazindua simu yake yenye mapinduzi yateknolojia ya juu katika kamera. “Ni kweli tutazindua simu ambayo tunaamini kwa watumiaji wa smartphone, hii itakuwa simu yenye teknolojia ya kisasa kabisa ambayo ndio mahitaji ya watumiaji walio wengi hasa wanaopenda kwenda sambamba na teknolojia” Amesema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TECNO. Kamera ya nyuma ya simuhiyo ambayo ina MP64 ina kamera nyingine mbili saidizi ambazo zina kazi tofauti, mathalani kazi ya kamera ya kwanza yenye MP5 ni kuongeza upana wa mazingira ya picha inapochukuliwa kwa zaidi ya 115˚ huku kamera yenye MP 2 ikisaidia kurembesha picha katika mitindo tofauti tofauti maarufu kama bokeh effects. Sifa ya kamera hii inafanya mtumiaji wa CAMON15 kuwa mpiga picha bora wakati wowote na mahali popote. Kameraya mbele yenyeukubwa wa MP32 imetengenezwa na kuwekwa ndanina huchomoza na kuonekana juu pindi tu mtumiaji anataka kupiga selfiekwa kifupi ni pop-up camera. Haijalishi ni Usiku au kuna mwanga hafifu kamera ya CAMON 15 ina uwezo wa kupiga picha inayong’ara kwenye mazingira yoyote. Upande wa sifa nyingine za CAMON15 ni pamoja na ukubwa wa kioo 6.6”FHD, betri yenye 4000mAh, ni laini mbili ambazo ni 4G pia ina android Q. Tayari mipango ya kuizindua kupitia mitandao ya kijamii imeshakamilika na wakati wowote simu hii itazinduliwa. Ikumbukwe TECNO ndio kampuni ya simu namba moja inayozalisha na kusambaza Smartphone huku toleo lake la mwisho kabisa katika mfululizo wa matoleo ya CAMON ni CAMON 12 series. Soma zote >>

Tetesi: Huenda TECNO ikatimiza mapinduzi haya ya teknolojia ya kamera ya simu 2020

waku7bisha | 2020-04-12101706

CAMON 15 Series
Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO ndio kampuniinayosemekana na wadadisi wa masuala ya teknolojia ya simu kuwa huenda ndioitakayoleta teknolojia ya kamera ya simu ambayo kwa mara ya kwanza katikatasnia ya masuala ya simu janja Tanzania itakata kiu kwa watumiaji wa simu hizohasa kwa upande wa kamera, betri na muundo wa simu yenyewe. Toleo la simu hiyo halijawekwa wazi bado lakiniimebainishwa kuwa litatoka kwenye mfululizo wa matoleo ya TECNO CAMON nalitaachiwa sokoni ndani ya mwezi huu Aprili. Simu hiyo imebainishwa itakuwa na kamera tatu nyumalensi na flash ambapo kamera kuu ina MP64. Teknolojia ya kamera ya simu hiiinaelezwa kuwa na uwezo wa kupiga pichamahali popote hata gizani kutokana na kuwa na flash nne zenye uwezo na nguvukubwa ya kusawazisha picha ing’are sehemu zenye ukungu na giza huku lensiyakeikimwezesha mtumiaji kupiga pichakitaalam zaidi hata kama hana ujuzi wa kupiga picha. Kwa taarifa zilizozagaa ni kwamba upande wa kamera yambele ina MP32 huku ikiwa tofauti kabisa namna ilivyoundwa kwani iko ndani yasimu ambapo mtumiaji akitaka kupiga selfie camera hii huchomoza kwa juu. TECNO ambayo simu yake ya mwisho katika mfululizo waCAMON ni CAMON12, ndio kampuni inayotarajiwa kuleta madiliko makubwa yateknolojia ya kamera za simu kwa mwako huu 2020. Kwa upande wa sifa nyingine endelea kufuatilia taarifazetu tutawapa mrejesho mara tu baada ya kupata taarifa rasmi kutoka TECNO. Soma zote >>

TECNO Yafungua Duka Kubwa la Kisasa Arusha

waku7bisha | 2020-02-1934446

General
Kampuni ya simu za mkononi TECNO imezindua duka kubwa la simu, maarufu ‘Smarthub’jijini Arusha ambalo linatoa hudumambalimbali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo mwishoni mwa wiki, Mwakilishi waMkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Benjamin Maneno ambaye piaalikuwa ndiye mgeni rasmi, alisema; “Kwa karne tuliyofikia hivi sasa, matumiziya smartphone hayaepukiki, kwahiyo tunachoomba sasa wananchi waje kwenye madukaya TECNO kwaajili ya kupata fursa ya kupata vipato kupitia simu za TECNO, siokutumia kuchati tu lakini unapotumia intaneti kwenye simu za TECNO unawezakufanya biashara na hata kupata masomo” Kwa upande wake Msimamizi wa Mauzokanda ya Kaskazini Bw. Kassim Haji alisema, “Tunawakaribisha wateja wa mikoa ya karibu katika Duka hili jipya la TECNO“Smart Hub”, Kuna faida nyingi ambazo wateja watanufaika nazo ikiwemo huduma yakupata fursa ya kununua bidhaa zetu za simu kwa bei nafuu, vifaa vya simu,kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi, sifa na mifumo ya simu, vilevilekwa mteja atakayenunua simu katika msimu huu wa Valentine, ataingia kwenye drooya kujishindia friji kubwa” Uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wadaumbalimbali wa TECNO uliambatana na burudani huku baadhi ya wadau wakipendekezamambo mbalimbali yanayohusu kupotea kwa simu. “Leo tunawashukuru sana uongozi mzima wa TECNO kwa kujali mahitaji yawananchi wa jiji la Arusha kuamua kufungua duka jipya la kisasa. Uongozi mzima waTECNO wajaribu kuwafundisha wananchi wanapokuja kununua simu mambo ya msingiwanayoweza kuhifadhi ili baadaye simu ikipotea waweze kui-track” Alisema mdauBw. Severine Kinabo. TECNO imedhamiria kupanua wigo wa huduma zake na kuzisogeza karibu na watejawake kwa kufungua maduka makubwa ya kisasa yenye huduma zote ambapo watejahawatatumia muda mrefu kupata huduma hizo. Hata hivyo TECNO tayari imeshaweka maduka makubwa katika majiji yote makubwaTanzania ikiwemo, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya. Soma zote >>

TECNO kutimiza Ndoto yako Valentine Day 2020

waku7bisha | 2020-02-1391598

General
Kuelekea kusherehekea siku ya wapendanao Februari 14, kampuni ya simu za mkononi TECNO, imeandaa mambo makubwa ambayo yatatimiza ndoto za wateja wake wengi watakaonunua simu za TECNO SPARK4, CAMON 12 na CAMON12 AIR,sio tu wateja hata wafuasi wake wa kurasa za TECNO mtandaoni watapata nafasi. Hapa kuna baadhi tu ya mamboyatakayofanywa na TECNO msimu huu wa Valentine. Kubwa kuliko ni kwamba imeandaliwa zawadi ya Chopper riding, zawadi hiini maalum kwaajili ya wateja watakaonunua simu tajwa pamojana fans wa kurasa za TECNO mtandaoni, hapa wateja hao watapewa nafasi ya kuruka na Helikopta ili kutazama mwonekano wa Jiji zima la Dar es Salaam bure kwa masaa kadhaa wakiwa angani. Vilevile TECNO itawakutanisha watu wawiliwawili wa jinsia tofauti bila wao kufahamianahii inajulikana kama Blind date nawatapambwa kwa mavazi na mwonekano kwa gharama za TECNO ambapo wanawake watarembwa na saluni ya viwango vya juu sana na wanaume watavalishwa mavazi na duka lenye hadhi kisha kupelekwa kwenye hoteli mojamaarufu yenye hadhi ya juu sana jijini Dar es Salaam kwaajili ya chakula cha jioniama dinner. Kujua zaidi tembelea Maduka ya TECNO au kurasa zao za Facebook, Twitter tecnomobiletanzania au follow Instagram https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/ Pamoja na hayo yote, TECNO pia imeandaa zawadi kemkem kwa wateja watakaonunua simu yoyote ya TECNO. Ikumbukwe kwamba Valentine ya mwaka 2019 TECNO iliwapeleka wateja na fans wake Visiwani Zanzibar kwaajili ya mapumziko na kutembelea maeneo maalum ya kitalii Soma zote >>

Shindano la 1st Valentine's Day Mobile Original Wallpaper linaendelea; Zawadi kubwa inakungojea

waku7bisha | 2020-02-1021447

General
Habari wapendwa! Siku yawapendanao iko njiani! Je Unajua kushiriki upendo tofauti? Wakati huu TECNOSPOT pamoja na Hi Theme imeandaa shindano la "1st Valentine's Day Mobile Original Wallpaper" kukusaidia kuwa na sikubora na maalum ya Valentine's Day. Bonyeza link hiyo na zoezi zima ili kushiriki na utengeneze wallpaper kali. Zawadi kubwa inakusubiri! https://spot.tecno.com/global/forum.php?mod=viewthread&tid=77376 Soma zote >>

Shukran za MbeyaConscious kwa TECNO Mobile Tanzania

waku7bisha | 2020-01-2822808

CAMON 12 Series
Siku chache baada ya mshindi wa kucomment sifa za TECNO Spot kupata zawadi yake, aliamua kuandika article humu akiishukuru kampuni ya TECNO Mobile Tanzania kwa kufanikisha ndoto zake kwa namna moja au nyingine. Kwenye article hiyo, ndugu Emanuael alisema yafuatayo: "Ni Lazima Nitoe Shukrani Za Dhati Kwa Kampuni Ya Tecno Mobile Tanzania Kwasababu Hizi Action movies Nafanyia Smartphone Device Aina Ya Tecno Mobile Tanzania Sasa Zimeanza Kupata Umaarufu Mkubwa Kwenye Mtandao Wa YouTube Sasa. Hii Ni Video Moja Ambayo Mpaka Sasa Inawatizamaji Laki Tatu Na Elfu Tisini Na Mbili" Soma zote >>

Mshindi wa shindano la kucomment sifa za TECNO Spot akiwa na simu yake

waku7bisha | 2020-01-2332665

CAMON 12 Series
Habari za January ndugu wanafamilia wa TECNO Spot. Natumai mnaendelea poa na pirika za hapa na pale Mnamo kuelekea mwishoni mwa mwaka 2019, version mpya ya TECNO Spot ilizinduliwa. Uzinduzi huo ulienda sambamba na shindano ambalo lilimtaka mtumiaji ajiunge kwenye forum na kucomment sifa za TECNO Spot version 2.0.0.2 ili apate nafasi ya kujishindia simu mpya ya Camon 12. Gusa hapa kwa maelezo zaidi kuhusiana na hilo shindano. Kama ilivyo kawaida ya TECNO kua wakiahidi wanatenda, mshindi wa shindano hilo ndugu Emmanuel Richard Mwaikuyu almaarufu kama Mbeya Conscious, mwenye TECNO Spot username @mbeyatexno alifikishiwa simu yake mpaka kwake Mbeya. Naye alikua na haya ya kusema, "Nashukuru sana, nimefurahi sana. Pia naamini action movies zangu nitazifanya vyema zaidi na kuitangaza brand ya TECNO kwenye mitandano yangu ya kijamii. Pia YouTube nawafahamisha watazamaji wa video zangu kwamba hua natumia smartphone device aina ya TECNO. Nawashukuru sana, tena sana" Soma zote >>
Watumiaji wanaopendekezwa
PROGRAMU YA TECNO SPOT

Changanua msimbo ili kupakua programu ya TECNO Spot

Shughuli Maarufu

© 2021 TECNO Mobile